Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein
akisalimiana na Padri Joseph Monesmo Magamba wa Kanisa la Romani
Katoliki Parokia ya Machui, alipofika katika Hospitali ya Mnazi Mmoja
kumpa pole Mjini Unguja,baada ya kumwagiwa tindikali na watu
wasiojulikana katika Mtaa wa Mlandege Mkoa wa Mjini Magharibi jana
jioni, Padri alimwagiwa Tindikali alipokuwa akitoka kupata huduma ya
Mtandao.
Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein
akimsikiliza Padri Joseph Monesmo Magamba,wa Kanisa la Romani Katoliki
Parokia ya Machui,akitoa maelezo jinsi alivyopata mkasa wa kutiwa
Tindikali jana na watu wasiojulikanwa,katika mtaa wa Mlandege Mjini
Unguja, alipofika katika Hospitali ya Mnazi Mmoja kumpa pole,ambapo
amelazwa na kuapatiwa matibabu.
Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed
Shein,akiwafariji jamaa na ndugu wa Padri Joseph Monesmo Magamba,wa
Kanisa la Romani Katoliki Parokia ya Machui,waliofika katika Hospitali
ya Mnazi Mmoja kumpa pole Padri huyo baada ya kumwagiwa Tindikali na
Watu wasiojulikanwa jana jioni Mtaa wa Mlandege Mjni.
Mmoja wa Ngugu wa
Padri Joseph Monesmo Magamba wa Kanisa la Romani Katoliki Parokia ya
Machui akimueleza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi
Dk.Ali Mohamed Shein,hisia zake kwa Uchungu kutokana na kitendo hicho
cha kumwagiwa Tindikali na watu wasiojulikanwa kwamba zilichukuliwe
hatua za kisheria na kukomeshwa Vitendo kama hivyo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akifafanua jambo wakati akiwafariji
jamaa na ndugu wa Padri Joseph Monesmo Magamba wa Kanisa la Romani
Katoliki Parokia ya Machui,waliofika kumuangalia Padri huyo aliyelazwa
katika Hospitali ya Mnazi Mmoja baada ya kumwagiwa Tindikali na Watu
wasijulikanwa jana jioni katika Mtaa wa Mlandege Mjini Unguja.(Picha na Ramadhan Othman wa Ikulu, Zanzibar).
0 comments:
Post a Comment