Kampuni ya simu ya mkononi ya Airtel kupitia huduma…
Waandishi wa habari waliohudhuria semina ya ya upigaji picha iliyodhaminiwa na kampuni ya simu ya Airtel jijini Dar Es Salaam.
Kampuni ya simu ya mkononi ya Airtel
kupitia huduma yake ya kibebki ya Airtel Money kwa mara ya pili
imedhamini semina ya wapiga picha wanahabari inayofanyika kwa muda wa
siku mbili hapa jijini Da r Es Salaam kuanzia leo 18 hadi 19 Apili 2012.
Airtel kupitia huduma yake ya Airtel Money imedhamini kampuni ya jijini Dar es salaam ijulikanayo kama MP5 2011 entertainment kuandaa semina maalum itakayowakutanisha wataalam na wapiga picha za habari wa muda mrefu kukutana na wanahabari wapiga picha ili kubadilishana uzoefu na kujifunza mambo mbalimbali kwa lengo la kuboresha utendaji kazi zao.

Akiongea kwa niaba ya waandishi wapiga
picha waliohudhuria semina hiyo Bw, Selemani Mpochi mpiga picha wa muda
mrefu nchini alisema “hii ni sehemu muhimu sana kwetu wanahabari
kujitengenezea utaratibu wakukaa pamoja na kutafakari mambo muhimu ili
kuendelea kufanya kazi zetu kwa ufanisi,Kwa niaba ya wenzangu wote
tunawashukuru sana Airtel kupitia huduma yao ya Airtel Money kwa
kutudhamini katika semina hii kwa mara ya pili sasa, tunashukuru sana
kwa ushirikiano wao wa kuwa tayari kutusaidia kuendeleza taaluma yetu na
kuonyesha kuwa wanatambua umuhimu wa wanahabari nchini
Airtel inaendelea kuboresha huduma ya
Airtel Money pesa mkononi na mpaka sasa watanzania wengi wamenufaika
kwani imeweza kutoa ajira kwa watanzania wengi kupitia uwakala hivyo
wananchi wengi wameweza kujipatia mapato kwa kupitia huduma hivyo semina
hii ni njia nyingine itakayoweza kuinua kiwango cha mapato na uelewa wa
Airtel Money kwa waandishi wa habari nchini
Zaidi ya wapiga picha za habari wapatao 15
toka vyombo vya habari nchini wanatarajiwa kuhudhuria semina hiyo jijini
Dar es salaam katika ukumbi wa msimbazi center
0 comments:
Post a Comment