Saturday, September 28, 2013

MKE WA RAIS MAMA SALMA KIKWETE AZURU NEBRASKA NCHINI MAREKANI

IMG_2914Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo,WAMA, Mama Salma Kikwete akipokewa na Founder, Benefactor and Chief Executive Officer wa Taasisi ya Opportunity Education Bwana Joe Ricketts kwenye uwanja wa ndege katika mji wa Omaha uliopo katika Jimbo la Nebraska nchini Marekani tarehe 27.9.2013 IMG_2917Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akipokea ua kutoka kwa binti Kate Stephens, 7, mara baada ya Mama Salma kutua kwenye uwanja wa ndege wa Omaha huko Nebraska nchiniMarekani tarehe 27.9.2013. IMG_2976Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akionyeshwa na Bwana James Ricketts, President and Chief Operations Officer, wa Taasisi ya Oppoturnity Education shughuli mbalimbali za kununua na kusafirisha vifaa vya elimu kwenda kwenye shule katika nchi mbalimbali hapa duniani ikiwamo Tanzania wakati Mama Salma alipotembelea Taasisi  hiyo yenye Makao Makuu yake huko Omaha katika Jimbo la Nebraska nchini Marekani tarehe 27.9..2013. IMG_2992Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo,WAMA, Mama Salma Kikwete akipokea zawadi ya ngao kutoka kwa Bwana Joe Ricketts, Founder, Benefactor and Chief Executive Officer wa Taasisi ya Opportunity Education iliyoko huko Omaha nchini Marekani. Bwana Ricketts alitoa zawadi hiyo kwa kutambua mchango mkubwa sana alioufanya Mama Salma binafsi na Taasisi yake ya WAMA Foundation katika masuala ya elimu. Afya na uwezeshaji kwa akina mama..
IMG_3016Mke wa Rais na Mwenyekiti wa WAMA, Mama Salma Kikwete akifanya mazungumzo na uongozi wa juu wa Taasisi ya Opportunies Education kwenye ofisi za taasisi hiyo huko Omaha Nebraska nchini Marekani tarehe 27.9.2013. IMG_3068 IMG_3074Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akikaribishwa kwenye Mji Mkuu wa Jimbo la Nebraska, Lincoln, huko Marekani na Dr. Natalie Hahn, Mwanzilishi wa Malaika Foundation na Senior Private Adviser for the United Nations Fund for International Partnership (UNFIP) tarehe 27.9.2013. IMG_3089Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akipokewa na Dr. Marjorie Kastelnik, Dean, College of Education and Human Sciences kwenye Chuo Kikuu cha Nebraska ambapo Mama Salma alishiriki kwenye Gala to support Global Education kwenye Chuo Kikuu cha Lincoln huko Nebraska tarehe 27.9.2013. IMG_3098Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akisalimiana na Mke wa Bwana Joe Ricketts kwenye gala  to support Global Education .
IMG_3139 Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akihutubia waalikwa waliohudhuria Gala to support Global Education iliyoandaliwa kwa ajili ya kumtunuku tuzo maalum Bwana Joe Ricketts kwa juhudi zake za kuboresha elimu duniani hasa katika nchi zinazoendelea.

0 comments: