Saturday, September 28, 2013

MAADHIMISHO YA MIAKA 18 YA KITUO CHA SHERIA NA HAKI ZA BINADAMU YAFANYIKA DAR

Dr. Ringo Tenga ambaye ni mmoja wa waasisi wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), akielezea historia ya kituo hicho. (wa kwanza kulia) ni Sengodo Mvungi ambaye pia ni muasisi wa kituo hicho.
 Kwaya iitwayo Mwalusanya inayoundwa na wafanyakazi wa kituo hicho, ikitumbuiza wakati wa maadhimisho hayo.…
Dr. Ringo Tenga ambaye ni mmoja wa waasisi wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), akielezea historia ya kituo hicho. (wa kwanza kulia) ni Sengodo Mvungi ambaye pia ni muasisi wa kituo hicho.
Kwaya iitwayo Mwalusanya inayoundwa na wafanyakazi wa kituo hicho, ikitumbuiza wakati wa maadhimisho hayo.
Wanafunzi walihodhuria sherehe hizo wakimsikiliza kwa makini, Dr.Ringo.
Baadhi ya wadau wa kituo hicho wakisikiliza kwa makini historia ya kituo hicho.
Mkurugenzi wa kituo hicho, Dr. Hellen Kijo-Bisimba akilishwa keki na Bumi Mwalusanya. (Nyuma kushoto ni Dr. Sengodo Mvungi na Dr. Ringo Tenga ambao ni miongoni mwa waasisi wa kituo hicho.
Dr. Sengodo Mvungi akilishwa keki na Bumi Mwalusanya kuashiria uzinduzi wa sherehe hizo. (Wa kwanza kushoto ni Mhe. Rozy Kamili Mbunge wa Viti Maalumu Chadema), Mhe, Kamili ni mmoja wa wajumbe wa Bodi ya (LHRC) wa muda mrefu.

Maadhimisho ya miaka 18 ya Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) yalifanyika juzi Septemba 26, jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na waasisi wa kituo hicho, wanachama, wanafunzi wa baadhi ya shule za Sekondari na msingi, viongozi wa dini na serikali na wadau wengine.
Wakati wa maadhimisho hayo yaliyofanyika Makao Makuu ya LHRC,  Kijitonyama, mmoja wa waasisi wake, Dr. Ringo Tenga alielezea historia ya kituo hicho kilichoanzishwa 1995 ambapo lengo lake ni kupambana na matukio ya uvunjivu wa haki za binadamu.
Mkurugenzi wa kituo hicho, Dr. Hellen Kijo-Bisimba akizungumza wakati wa maadhimisho hayo alisema licha ya  kukumbana na changamoto nyingi, kituo chao kimepata mafanikio mengi.
Aliyetaja baadhi ya mafanikio hayo kuwa ni kuweza kuwatetea watu ambao kwa namna moja au nyingine hawakutendewa haki.
Mmoja wa watu aliyekuwa wa kwanza kutetewa na kituo hicho alikuwa marehemu Adam Mwaibabile aliyekuwa Mwandishi wa Habari wa Gazeti la Nipashe na Radio One mkoani Ruvuma.
Alisema baada ya mwandishi huyo kufungwa kwa uonevu, walikwenda Ruvuma ambapo walimpigania na kufanikiwa kumtoa katika kifungo alichohukumiwa na matukio mengine.
Kuhusu changamoto wanazokutananazo alisema ni kunyimwa vibali vya kufanya kazi na baadhi ya watendaji wa serikali wanapokwenda mikoani, kuitwa wanasiasa wa Chadema, chama cha kidini nk.
Zifuatazo ni baadhi ya picha za matukio yaliyojiri wakati wa maadhimisho hayo.

0 comments: