
Bumbuwazi: Meneja Everson Makowa-Mwale (49), akiwa ameduwaa baada ya kunaswa akijivinjari na mke wa mfanyakazi wake.
NI aibu kubwa kuliko
maelezo! Meneja wa kampuni ya kusafirisha mizigo ya Malawi Cargo, tawi
la mkoani hapa, Everson Makowa-Mwale (49), raia wa nchi jirani ya
Malawi amenaswa chumbani na mke wa mfanyakazi wake (jina tunalo).
Tukio hilo lililojaa fedheha lilitokea mwishoni mwa wiki iliyopita,
majira ya saa 11:25 jioni baada ya askari wa jeshi la polisi, ndugu na
jamaa kufika eneo la hoteli moja maarufu jijini hapa (jina
limehifadhiwa) na kumkuta chumbani akiwa mtupu akijiandaa kufanya ngono
na mke huyo wa mtu.
Ilidaiwa kuwa mtuhumiwa huyo, kabla ya
kuumbuka, alikuwa ameandaa mazingira yote kwa ajili ya kuvunja amri ya
sita na mke huyo wa mfanyakazi wake.
Mtego wa kumnasa ulifanikiwa
baada ya mtuhumiwa kutinga hotelini hapo akiwa na gari la kampuni aina
ya Toyota Hilux lenye namba za usajili T 821 ASY na kunyooka moja kwa
moja chumbani alikokuwa akisubiriwa na mwanamke huyo.
WASIFU WA MENEJA
Habari za uhakika zilieleza kuwa bosi huyo ni mbunge mstaafu aliyewahi
kuwa Mheshimiwa wa Jimbo la Nkotakota South East nchini Malawi kwa
kipindi cha miaka kadhaa.
Jamaa huyo aliangushwa na Agness Chatipwa
Mandebvu katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2009 nchini humo ndipo akatinga
jijini hapa na kupata kazi ya umeneja wa kampuni hiyo ya usafirishaji.
MADAI MAZITO
Ilidaiwa kuwa meneja huyo ndiyo mchezo wake kwa sababu amekuwa
akiwafanyia hivyo mabinti wanaofika ofisini kwake kwa ajili ya kuomba
kazi ambapo huwakubalia kuwapa kazi endapo watakubali kushiriki naye
dhambi ya uzinzi.
Uchunguzi ndani ya kampuni hiyo ulidaka madai
kuwa tangu awe meneja, mabinti zaidi ya watano waliacha au kufukuzwa
kazi walipokataa kufanya naye ngono.
Ilidaiwa kuwa wanaokubaliana na hali hiyo kutokana na ugumu wa maisha humkubalia na kupandishwa vyeo kiholela.
Sakata la tabia hiyo chafu kwa raia wa Kitanzania, lilifikia kikomo
baada ya mfanyakazi mmoja (jina limehifadhiwa) ambaye alikuwa ni
mfanyakazi wa ndani wa meneja huyo kusimamishwa kazi kwa madai kuwa
alichelewa kuripoti kazini.
MCHEZO WA NIPE NIKUPE
Mfanyakazi huyo ambaye alikuwa akiishi na mkewe nyumbani kwa bosi wake,
alisimamishwa kazi ambapo bosi huyo alitumia mwanya huo kuanza
kumchombeza mke wa jamaa huyo kwa kumwambia amkubalie ili amrudishe
mumewe kazini.
Baada ya kupata usumbufu huo kwa kipindi kirefu
ndipo jamaa huyo pamoja na wafanyakazi wenzake ambao walikuwa
hawaipendi tabia ya bosi wao wakaandaa mtego uliomnasa kama panya bila
kujinasua na kuishia mikononi mwa polisi.
WAFANYAKAZI
Taarifa zilizothibitishwa na baadhi ya watumishi wa kampuni hiyo ambao
majina yake hawakutaka yaandikwe gazetini, walisema tabia ya bosi wao
imekithiri na kwamba amekuwa akitumia wadhifa wake kuwalaghai watoto wa
kike ili kufanya nao mapenzi.
Wafanyakazi hao walidai ni bora Idara
ya Uhamiaji mkoani hapa iingilie kati suala hilo ili kuwanusuru
Watanzania dhidi ya watumishi wa kigeni wanaokuwa na tabia zinazolenga
kuwaondolea utu wao.
TURUDI KWENYE TUKIO
Baada ya kufumaniwa akiwa mtupu kutokana na mke wa mtu huyo kutoa
ishara kwa walioweka mtego, aliomba radhi kwa mume wa mwanamke huyo
ambaye ni mwajiriwa wa kampuni anayefanya kazi ya kutengeneza bustani.
Hata hivyo, msamaha wake ulikataliwa na soo likatinga polisi na sasa anasubiriwa kupelekwa mbele ya mkono wa sheria...