INATISHA na hofu kubwa imetanda katika Kijiji cha Kimange, Wilaya ya
Bagamoyo mkoani Pwani kufuatia baadhi ya viongozi wa dini kuwatumia
vijana wa hapo kama misukule ili wapelekwe kanisani.
Msukule.
Uchunguzi wa gazeti hili umebaini kuwa nia ya viongozi hao wa dini
kuteua kijiji hicho na kuwatumia vijana wa hapo kama misukule ni
kuwalaghai waumini kwamba wana uwezo wa kufufua watu wanaodaiwa kufa na
kuchukuliwa kimazingara.
Gazeti hili limebaini kuwa viongozi hao
wa dini wamekuwa wakifanya udanganyifu huo lengo lao likiwa ni kupata
waumini wengi katika makanisa yao ambao wamekuwa wakiamini kwamba kweli
misukule inarejeshwa katika maisha…
Na Makongoro Oging', BagamoyoINATISHA
na hofu kubwa imetanda katika Kijiji cha Kimange, Wilaya ya Bagamoyo
mkoani Pwani kufuatia baadhi ya viongozi wa dini kuwatumia vijana wa
hapo kama misukule ili wapelekwe kanisani.
Msukule.
Uchunguzi wa gazeti hili umebaini kuwa nia ya viongozi hao wa dini
kuteua kijiji hicho na kuwatumia vijana wa hapo kama misukule ni
kuwalaghai waumini kwamba wana uwezo wa kufufua watu wanaodaiwa kufa na
kuchukuliwa kimazingara.
Gazeti hili limebaini kuwa viongozi hao wa
dini wamekuwa wakifanya udanganyifu huo lengo lao likiwa ni kupata
waumini wengi katika makanisa yao ambao wamekuwa wakiamini kwamba kweli
misukule inarejeshwa katika maisha ya kawaida.
Habari kutoka kijijini
hapo zinadai kwamba viongozi wa dini wanaofika katika kijiji hicho
wamekuwa wakiwalipa watu wanaojitokeza kuwa misukule bandia kati ya
shilingi 200,000 hadi 250,000 kwa kila mtu.
Msukule.
Imegundulika kuwa viongozi hao wa dini hufanya zoezi hilo kwa siri
kubwa na kuna nyumba ya mchungaji mmoja, nje kidogo ya kijiji hicho
ambapo misukule hao feki hupewa mafunzo ya nini cha kufanya kabla ya
kusafirishwa kuelekea Dar es Saalam.
Imeelezwa kuwa misukule
husafirishwa kwenye magari yenye vioo vyeusi ‘tinted’ wakiwa wamepakwa
matope mwili mzima na kuvalishwa nguo zilizochanika.
“Wapo
wachungaji waliofanya hivyo kwa kuwalaghai waumini wao kwamba wana uwezo
wa kufufua watu huku wakijua kwamba lengo lao ni kuwavutia watu
wajazane kwenye makanisa yao ili wapate sadaka nyingi,” kilisema chanzo
chetu.
Uchunguzi umebaini kwamba kuna makanisa ambayo yana
wafuasi wengi wa kufanya mazingaombwe ya namna hiyo na wamekuwa
wakijipatia fedha nyingi ambapo kwa Jumapili moja, hujikusanyia kati ya
shilingi 7,000,000 hadi 7,500,000.
Aidha, ‘hukomba’ sadaka wakati wa maombi ya katikati ya wiki kwa kutumia mbinu mbalimbali za kuvuta waumini.
Baadhi
ya vijana wa kijiji hicho ambao waliwahi kurubuniwa na wachungaji
baada ya kufuatwa kijijini hapo ni pamoja na Ziada Mlanga (33) na
Shakila Ayubu (29).

Katika mahojiano na mwandishi wetu kijijini hapo, Ziada alikuwa na haya ya kusema:
“Machi
21, 2011 kaka mmoja (jina tunalihifadhi) anayeishi Kijiji cha Makore
jirani na chetu, alinifuata na kunieleza kwamba anahitaji vijana wanne,
wa kike wawili na wa kiume wawili ili wajiunge katika shughuli za
sanaa, yaani kuigiza.
“Hata hivyo, alifanikiwa kunipata mimi na
Shakila, akatuahidi kutulipa shilingi 350,000 kila mmoja na wazazi wetu
kupewa shilingi 100,000 kila mmoja.
“Tulikubali kufanya hivyo,
walituchukua kwa pikipiki hadi Kijiji cha Makore nyumbani kwa mtu mmoja
aliyemtaja kuwa ni mchungaji.
“Tulipofika huko walituweka katika
chumba maalum katika nyumba ya huyo mchungaji ambayo ipo porini,
wakatueleza kwamba tusubiri kuna watu wanakuja kutupa mafunzo.
“Baada
ya muda mfupi walifika watu ambao tulipoongea nao, walitueleza tuvue
nguo zote tubaki na za ndani. Tulifanya hivyo, wakatupaka majivu,
wakatuvuruga nywele na kutuvalisha nguo chakavu na ilipofika saa moja
usiku, walikuja watu wengine wakiwa kwenye gari yenye vioo vya tinted.
“Walitueleza
kwamba tunaelekea jijini Dar es Salaam ambako tukifika tujifanye
mazezeta. Tulifika usiku sana na kupelekwa katika kanisa moja (jina
linahifadhiwa).
“Ndani ya gari lile kulikuwa na bastola, hatukujua ni
ya nini, pale kanisani tulitengenezewa chai. Hata hivyo, tulikataa
kuinywa.
“Baadaye walitueleza kwamba wametufanya vile ili tuonekane
kama watu waliokuwa wamechukuliwa kimazingara na kufanywa misukule na
sasa tumeokolewa na mchungaji wa kanisa hilo.
“Kesho yake ilikuwa
Jumapili, tuliambiwa tutasimama mbele ya waumini kanisani na tusiseme
kitu chochote ili tuje kuanza kuongea kidogo baada ya kuombewa na
mchungaji.
“Hata hivyo, tulipewa majina ya watu mashuhuri waliokufa
lakini mimi nilikataa kwa kuwa aliyetajwa kuwa nijifanye ndiyo mimi
alikuwa mtu maarufu.
“Nilijiuliza ndugu zake wangenielewaje? Kitu
cha pili ni kwamba nilikataa kwa kuwa fedha tulizokubaliana walikuwa
hawajatupatia na tukaona kuwa huo ni udhalilishaji.
“Baada ya kuona
tumekataa, walitusihi tusitoe siri na baadaye tulipewa nguo nyingine
tukavaa na tukapewa shilingi elfu hamsini kila mmoja kama nauli ya
kurudia kijijini kwetu Kimange.
“Tulipofika tuliwaeleza wazazi wetu
mambo tuliyofanyiwa wakaona tumedhalilishwa, ikabidi tuje nao Dar es
Salaam tukaenda hadi Kituo cha Polisi Magomeni na kufungua kesi.
“Tuliwaambia polisi kuwa simu na nguo zetu ziko kwa watu hao lakini
hadi leo kesi tuliyofungua hatujui ilipofikia na tuliambiwa polisi
wamewasiliana na wenzao wa Mkoa wa Pwani.
“Polisi wa Pwani walikuja
Dar na kutuchukua hadi Kibaha ambako tulitoa maelezo na tukaenda nao
Kijiji cha Makore lakini hatukumkuta mchungaji huyo, tukaambiwa kuwa
alihama baada ya kupata habari kuwa anatafutwa na polisi,” alisema Ziada
akiungwa mkono na Shakila.
BABA WA ZIADA
Baba wa Ziada
aliyejitambulisha kwa jina la Sijali Musini Mlanga, alisema kwamba
kitendo walichofanyiwa watoto hao ni cha udhalilishaji na anaiomba
serikali kuchukua hatua.
“Hatuwezi kukubaliana na hali hiyo, huo ni
utapeli na udhalilishaji mkubwa, hakuna dini inayoweza kufanya mambo
kama hayo, wahusika wachukuliwe hatua,” alisema Mlanga.
MWENYEKITI WA KIJIJI
Mwenyekiti wa Kijiji cha Kimange, Juma Issa Madinga amekiri kufahamu suala hilo na kukemea kitendo hicho.
“Hao
wachungaji hawawezi kuachwa wakifanya mambo hayo na kusababisha kijiji
kupakaziwa kuwa ni cha misukule, sasa wananchi wasilaghaiwe na matapeli
hao, wakija tena watoe taarifa kwangu,” alisema mwenyekiti huyo.