This is default featured slide 1 title
Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.
This is default featured slide 2 title
Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.
This is default featured slide 3 title
Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.
This is default featured slide 4 title
Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.
This is default featured slide 5 title
Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.
Tuesday, April 2, 2013
UKWELI KAMILI NI HUU
JENGO lenye urefu wa ghorofa 16, lililoanguka katikati ya Jiji la Dar es Salaam na kusababisha vifo, ulemavu wa watu pamoja na uharibifu wa mali, lilikuwa lazima lianguke.
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete na Mke wake Mama Salma Kikwete wakiwa katika wodi
ya Taasisi ya Mifupa ya MOI katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili
jijini Dar es Salaam wakimpa pole kijana Mohamed Ally Dhamji ambaye ni
miongoni mwa majeruhi walionusurika katika jengo lililoporomoka
katikati ya jiji Ijumaa iliyopita na kusababisha vifo vya watu 34.
(PICHA NA…Kwa mujibu wa mhandisi wa majengo, Abel Kadali, anayemiliki kampuni yake, akiwa ni msomi mwenye shahada mbili, ujenzi wa jengo hilo, ulizungukwa na utani mwingi.
“Kwanza jengo refu kama lile linapokatika na kubomoka kisha eneo kugeuka kifusi kama hivi, maana yake ujenzi ulikuwa dhaifu kuanzia mwanzo hadi mwisho.
“Kama ujenzi ungekuwa mzuri, hili jengo hata kama lingeanguka, lisingesambaratika kama hivi. Hapa kuna kasoro za kiweledi. Ujenzi wa namna hii, huwa unatufanya tuonekane hatuwezi kazi,” alisema.
Macho ya waandishi wetu yaliona lakini Kadali akafafanua kwamba ni kosa kubwa kujenga ghorofa, halafu ukabana saruji.
“Nikishika tofali, naona ni mchanga mtupu. Kwa kadirio la kitaalamu, inaonekana kila mfuko mmoja wa saruji, ulitengeneza matofali 90. Maana ni mchanga mtupu.
“Kwa hiyo kosa la kwanza kabisa ninaloweza kuliona hapa ni matumizi ya saruji,” alisema Kadali.
NONDO DHAIFU
Kadali alifafanua kuwa nondo zilizotumika siyo za kujengea ghorofa lenye urefu huo.
“Nikiziangalia hizi nondo, naona kabisa hili jengo lilijengwa chini ya kiwango kuanzia kwenye msingi wake mpaka hapo lilipofikia na kuanguka. Sasa ni kwa nini lisianguke?
“Tunacheza na maisha ya watu. Nondo ni nyembamba sana, nikiziangalia, zinaonesha kuwa pamoja na wembamba wake, hazina ubora,” alisema Kadali.
TATIZO LA MALIGHAFI
Kuhusu ubora wa nondo, Kadali alisema kuwa inashangaza kuona zikikunjwa zinakatika.
“Hili ni tatizo la malighafi, lazima ukaguzi wa kina ufanyike kwenye viwanda vyetu, kuona ubora wa bidhaa zinazotengenezwa.
“Ni kweli nondo ni nyembamba lakini ukweli usipindishwe kuwa hata ubora wenyewe haupo. Ina maana zilitengenezwa kwa malighafi zisizokidhi viwango.
“Viwanda vyetu vinaunda nondo kwa kuyeyusha vyuma chakavu. Ni kosa kubwa. Wakati mwingine inakuwa siyo vyuma peke yake, bali ni mchanganyiko na ‘Alminiamu’,” alisema Kadali na kuongeza:
“Kama nondo inatengenezwa kwa kuchanganya chuma na Alminiamu, unatarajia kweli kupata nondo imara? Ifahamike kwamba kila madini na kazi yake.”
KOSA LA TBS
Kadali alisema kuwa kiwango dhaifu cha nondo na bidhaa mbalimbali nchini, ni matokeo ya Shirika la Viwango Tanzania (TBS) kutofanya kazi zake ipasavyo.
“Kuruhusu nondo kama zile kuingia sokoni na kuuzwa kwa ajili ya ujenzi, ni tatizo. TBS lazima wasimame imara kuhakikisha wanafanya kazi yao kisheria, hivyo kuokoa maisha ya Watanzania,” alisema Kadali.
KOSA LA NHC
Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), nalo limeingia lawamani kwa sababu kisheria, lenyewe lina haki katika umiliki wa jengo hilo lililoanguka.
NHC, linamiliki asilimia 25 ya hisa za jengo hilo, hivyo kitendo cha kuacha ujenzi holela, siyo tu kwamba limeshindwa kutimiza wajibu wake, bali pia linachezea rasilimali za Watanzania.
MAITI ZAFIKIA 34
Mpaka gazeti hili linaingia mtamboni, maiti zilizokuwa zimepatikana ni 30 na jitihada za kuendelea kusaka maiti zaidi zilikuwa zinaendelea.
Kamanda wa Polisi, Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Suleiman Kova alisema: “Uokoaji bado unaendelea, vyombo vyote vya dola vipo, pamoja na zana zote.”
WANANE WAKAMATWA
Kova alisema: “Mpaka sasa, polisi kanda maalum imeshawakamata watu wanane kuhusiana na kuanguka kwa ghorofa hilo.
“Waliokamatwa ndiyo waliohusika moja kwa moja, kuanzia michoro mpaka ujenzi. Kwa sasa nisingependa kuwataja majina kwa sababu uchunguzi unaendelea,” alisema Kova.
Kwa upande mwingine, Kova alisema: “Kipindi hiki tunaendelea na uokoaji, hatutarajii kupata majeruhi. Tunachofanya ni kuhakikisha tunapata maiti wote ili waweze kuzikwa kwa heshima zote kama binadamu.”
KUHUSU JENGO PACHA
Habari zinasema kuwa jengo hilo lililoanguka, lilikuwa na pacha wake, jirani kabisa na ilipo Hospitali ya Burhani. Kova amesema kuwa ujenzi wake umesimamishwa mara moja.
“Tuligundua kuwa mmiliki na mjenzi ni yuleyule, kwa hiyo tumechukua hatua za haraka sana kuzuia shughuli zote za ujenzi wa jengo hilo pacha,” alisema Kova.
JENGO lenye urefu wa ghorofa 16, lililoanguka katikati ya Jiji la Dar es Salaam na kusababisha vifo, ulemavu wa watu pamoja na uharibifu wa mali, lilikuwa lazima lianguke.
KIJIJI CHA MISUKULE CHAFUMULIWA
INATISHA na hofu kubwa imetanda katika Kijiji cha Kimange, Wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani kufuatia baadhi ya viongozi wa dini kuwatumia vijana wa hapo kama misukule ili wapelekwe kanisani.
Gazeti hili limebaini kuwa viongozi hao wa dini wamekuwa wakifanya udanganyifu huo lengo lao likiwa ni kupata waumini wengi katika makanisa yao ambao wamekuwa wakiamini kwamba kweli misukule inarejeshwa katika maisha…
Na Makongoro Oging', Bagamoyo
INATISHA na hofu kubwa imetanda katika Kijiji cha Kimange, Wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani kufuatia baadhi ya viongozi wa dini kuwatumia vijana wa hapo kama misukule ili wapelekwe kanisani.
Gazeti hili limebaini kuwa viongozi hao wa dini wamekuwa wakifanya udanganyifu huo lengo lao likiwa ni kupata waumini wengi katika makanisa yao ambao wamekuwa wakiamini kwamba kweli misukule inarejeshwa katika maisha ya kawaida.
Habari kutoka kijijini hapo zinadai kwamba viongozi wa dini wanaofika katika kijiji hicho wamekuwa wakiwalipa watu wanaojitokeza kuwa misukule bandia kati ya shilingi 200,000 hadi 250,000 kwa kila mtu.
Imeelezwa kuwa misukule husafirishwa kwenye magari yenye vioo vyeusi ‘tinted’ wakiwa wamepakwa matope mwili mzima na kuvalishwa nguo zilizochanika.
“Wapo wachungaji waliofanya hivyo kwa kuwalaghai waumini wao kwamba wana uwezo wa kufufua watu huku wakijua kwamba lengo lao ni kuwavutia watu wajazane kwenye makanisa yao ili wapate sadaka nyingi,” kilisema chanzo chetu.
Uchunguzi umebaini kwamba kuna makanisa ambayo yana wafuasi wengi wa kufanya mazingaombwe ya namna hiyo na wamekuwa wakijipatia fedha nyingi ambapo kwa Jumapili moja, hujikusanyia kati ya shilingi 7,000,000 hadi 7,500,000.
Aidha, ‘hukomba’ sadaka wakati wa maombi ya katikati ya wiki kwa kutumia mbinu mbalimbali za kuvuta waumini.
Baadhi ya vijana wa kijiji hicho ambao waliwahi kurubuniwa na wachungaji baada ya kufuatwa kijijini hapo ni pamoja na Ziada Mlanga (33) na Shakila Ayubu (29).
“Machi 21, 2011 kaka mmoja (jina tunalihifadhi) anayeishi Kijiji cha Makore jirani na chetu, alinifuata na kunieleza kwamba anahitaji vijana wanne, wa kike wawili na wa kiume wawili ili wajiunge katika shughuli za sanaa, yaani kuigiza.
“Hata hivyo, alifanikiwa kunipata mimi na Shakila, akatuahidi kutulipa shilingi 350,000 kila mmoja na wazazi wetu kupewa shilingi 100,000 kila mmoja.
“Tulikubali kufanya hivyo, walituchukua kwa pikipiki hadi Kijiji cha Makore nyumbani kwa mtu mmoja aliyemtaja kuwa ni mchungaji.
“Tulipofika huko walituweka katika chumba maalum katika nyumba ya huyo mchungaji ambayo ipo porini, wakatueleza kwamba tusubiri kuna watu wanakuja kutupa mafunzo.
“Baada ya muda mfupi walifika watu ambao tulipoongea nao, walitueleza tuvue nguo zote tubaki na za ndani. Tulifanya hivyo, wakatupaka majivu, wakatuvuruga nywele na kutuvalisha nguo chakavu na ilipofika saa moja usiku, walikuja watu wengine wakiwa kwenye gari yenye vioo vya tinted.
“Walitueleza kwamba tunaelekea jijini Dar es Salaam ambako tukifika tujifanye mazezeta. Tulifika usiku sana na kupelekwa katika kanisa moja (jina linahifadhiwa).
“Ndani ya gari lile kulikuwa na bastola, hatukujua ni ya nini, pale kanisani tulitengenezewa chai. Hata hivyo, tulikataa kuinywa.
“Baadaye walitueleza kwamba wametufanya vile ili tuonekane kama watu waliokuwa wamechukuliwa kimazingara na kufanywa misukule na sasa tumeokolewa na mchungaji wa kanisa hilo.
“Kesho yake ilikuwa Jumapili, tuliambiwa tutasimama mbele ya waumini kanisani na tusiseme kitu chochote ili tuje kuanza kuongea kidogo baada ya kuombewa na mchungaji.
“Hata hivyo, tulipewa majina ya watu mashuhuri waliokufa lakini mimi nilikataa kwa kuwa aliyetajwa kuwa nijifanye ndiyo mimi alikuwa mtu maarufu.
“Nilijiuliza ndugu zake wangenielewaje? Kitu cha pili ni kwamba nilikataa kwa kuwa fedha tulizokubaliana walikuwa hawajatupatia na tukaona kuwa huo ni udhalilishaji.
“Baada ya kuona tumekataa, walitusihi tusitoe siri na baadaye tulipewa nguo nyingine tukavaa na tukapewa shilingi elfu hamsini kila mmoja kama nauli ya kurudia kijijini kwetu Kimange.
“Tulipofika tuliwaeleza wazazi wetu mambo tuliyofanyiwa wakaona tumedhalilishwa, ikabidi tuje nao Dar es Salaam tukaenda hadi Kituo cha Polisi Magomeni na kufungua kesi.
“Tuliwaambia polisi kuwa simu na nguo zetu ziko kwa watu hao lakini hadi leo kesi tuliyofungua hatujui ilipofikia na tuliambiwa polisi wamewasiliana na wenzao wa Mkoa wa Pwani.
“Polisi wa Pwani walikuja Dar na kutuchukua hadi Kibaha ambako tulitoa maelezo na tukaenda nao Kijiji cha Makore lakini hatukumkuta mchungaji huyo, tukaambiwa kuwa alihama baada ya kupata habari kuwa anatafutwa na polisi,” alisema Ziada akiungwa mkono na Shakila.
BABA WA ZIADA
Baba wa Ziada aliyejitambulisha kwa jina la Sijali Musini Mlanga, alisema kwamba kitendo walichofanyiwa watoto hao ni cha udhalilishaji na anaiomba serikali kuchukua hatua.
“Hatuwezi kukubaliana na hali hiyo, huo ni utapeli na udhalilishaji mkubwa, hakuna dini inayoweza kufanya mambo kama hayo, wahusika wachukuliwe hatua,” alisema Mlanga.
MWENYEKITI WA KIJIJI
Mwenyekiti wa Kijiji cha Kimange, Juma Issa Madinga amekiri kufahamu suala hilo na kukemea kitendo hicho.
“Hao wachungaji hawawezi kuachwa wakifanya mambo hayo na kusababisha kijiji kupakaziwa kuwa ni cha misukule, sasa wananchi wasilaghaiwe na matapeli hao, wakija tena watoe taarifa kwangu,” alisema mwenyekiti huyo.
Saturday, March 30, 2013
MAHAKAMA YASEMA Uchaguzi Kenya ulikuwa huru na wa haki
Uamuzi huu una maana kuwa Uhuru Kenyatta ndiye ataapishwa kama rais mpya wa Kenya tarehe tisa mwezi ujao
Kesi hiyo iliwasilishwa katika mahakama ya juu zaidi na mpinzani mkuu wa Kenyatta, Raila Odinga baada ya uchaguzi uliofanyika mapema mwezi huu.
Matokeo rasmi yalionyesha kuwa Uhuru alishinda uchaguzi kwa kumpiku Raila kwa asilimia 50.07 huku Raila akipata asilimia 43.28. Matokeo haya yalizuia kufanyika kwa duuru ya pili ya uchaguzi kwa kura 8,100.
Bwana Odinga aliishutumu tume huru ya uchaguzi na mipaka kwa kuhujumu matokeo ya uchaguzi ili kumpa ushindi Uhuru Kenyatta.
Uchaguzi wa urais, wabunge na wajumbe wengine wa serikali, ulifanyika tarehe nne mwezi Machi, ukiwa wa kwanza tangu uchaguzi uliokumbwa na ghasia mwaka 2007 na kusababisha vifo vya watu zaidi ya elfu moja.
Bwana Kenyatta na mgombea mwenza wake ,William Ruto,wanakabiliwa na kesi katika mahakama ya jinai kwa kuchochea ghasia za mwaka 2007. Hata hivyo wamekanusha vikali mashtaka.
Mahakama ya juu zaidi inaweza kuthibitisha ushindi wa Kenyatta au kuubatilisha uamuzi wa wakenya na hivyo kuitisha uchaguzi mpya.Vyovyote matokeo yatakavyokuwa kuna wale watakaoghadhabika mno.
Rais anayeondoka mamlakani, Mwai Kibaki amewataka wakenya kuwa watulivu na kukubali uamuzi wa mahakama lakini wengi wanatagemea sana idara ya mahakama ambayo imekuwa na mageuzi makubwa na ambayo sasa watu watu imani nayo.
Mawakili wa Odinga wanasema kuwa kesi yao ilihusisha madai ya kuhujumu hesabu ya kura pamoja na matatizo ya usajili wa wapiga kura na vile vile matatizo ya mitambo ya usajili wa wapiga kura.
Mnamo Ijumaa mahakama ya juu zaidi ilidurusu matokeo ya kura katika vituo 22 vya kupigia kura. Na pande zote mbili zilisema matokeo yalithibitisha misimamo yao.
Kenyatta ameutaja uchaguzi huo kama ishara ya kukuwa kwa demokrasia Kenya na ulifanywa kwa njia ya amani.
Tume ya uchaguzi, pia imesisitiza kuwa uchaguzi ulikuwa huru licha ya hitilafu za kimitambo....
Wachunguzi wa kimataifa nao walisema kuwa uchaguzi ulikuwa huru na wa haki na kuwa tume huru ya uchaguzi uliendesha uchaguzi huo kwa uwazi.
MAUNO YA AUNTY LULU NUSURA YAUE
SI mnalikumbuka lile wowowo la Lulu Mathias Semagongo au Aunty Lulu? Si mnakumbuka jinsi mwenyewe anavyolisifia kwamba analipenda sana na siku akiamka akakuta halipo atakwenda kwa mchungaji aombewe? Sasa safari hii nusura liue. Twende pamoja.…
SI mnalikumbuka lile wowowo la Lulu Mathias Semagongo au Aunty Lulu? Si mnakumbuka jinsi mwenyewe anavyolisifia kwamba analipenda sana na siku akiamka akakuta halipo atakwenda kwa mchungaji aombewe? Sasa safari hii nusura liue. Twende pamoja.
Mkasa huo ulijiri kwenye sherehe ndogo ya watu wa karibu baada ya msanii wa filamu Bongo, Jacqueline Pentzel ‘Jack Chuz’ kufunga ndoa na Gardner Dibibi, Kinondoni, Dar es Salaam wiki iliyopita.
Ilikuwa ni wakati wa ndugu, jamaa na marafiki wakipata msosi sanjari na vinywaji huku muziki ukipigwa nyumbani kwa familia ya bibi harusi, Kinondoni, ndipo Aunty Lulu alipoanza kukata mauno na kushangiliwa.
Wakati watu wakimpa dole Aunty Lulu, jamaa huyo alimtolea macho pima na kuanza kuchanganyikiwa na mauno hayo.
Polepole jamaa, mkono mmoja ukiwa umeshika sahani yenye msosi mwingine soda, aliganda kwa sekunde kadhaa kama vile haamini anachokiona.
Kufumba na kufumbua, njemba alikwenda chini ghafla na kupoteza fahamu.
Hali ya hewa ilichafuka kuanzia hapo, ikawa patashika nguo kuchanika.
Hata hivyo, wanaume majasiri waliokuwa eneo la tukio walimpepea jamaa huyo ambapo baadaye alizinduka.
Jamaa huyo baada ya kurejewa na fahamu alisikika akisema: Ukweli wowowo la huyu dada (Aunty Lulu) limenichanganya, nusu linitoe roho jamani.
Baadhi ya watu walioshuhudia tukio hilo walisema kilichomtokea jamaa huyo ni mfadhaiko.












