Friday, September 13, 2013

HONGERA KWA KUJIUNGA NA TAIFA STAR

Adam Nditi.

WATANZANIA wawili wenye uraia wa Uingereza, wamekubali kurejea nchini kuichezea timu ya taifa, Taifa Stars.
Adam Nditi anayekipiga timu ya vijana ya Chelsea, mwenye uraia wa England, amesema yupo tayari kuitumikia Stars kama ilivyo kwa Ismail Feruz raia wa Scotland. Kocha Mkuu wa Stars, Kim Poulsen amesema wachezaji hao wawili makinda wamekubali kuichezea Stars.
 “Wote nimezungumza nao na wameonyesha wanataka kuja kuitumikia Taifa Stars badala ya Uingereza. Wako tayari kuja kuitumikia Tanzania ambayo ni nchi ya asili yao.
“Nditi amenifafanulia kwa nini alichukua pasi ya kusafiria ya England, lakini ana mapenzi makubwa na Tanzania.
“Hili si suala la TFF sasa, linakwenda zaidi katika siasa kama Tanzania itakubali kubadili mfumo na kuruhusu pasi mbili za kusafiria. Hii itatusaidia sisi.”

0 comments: