Friday, July 26, 2013

RAIS JAKAYA KIKWETE AKIWA WILAYANI MULEBA

Rais Kikwete akivikwa skafu na skauti baada ya kuwasili Muleba.

Vikundi vya ngoma vikitumbuiza wageni.…

Rais Kikwete akivikwa skafu na skauti baada ya kuwasili Muleba.
Vikundi vya ngoma vikitumbuiza wageni.
Rais Kikwete akisalimiana na mama wa Profesa Anna Tibaijuka.
Waziri wa Ardhi Profesa Anna Tibaijuka akishiriki katika ngoma ya utamaduni wakati wa mapokezi ya Rais Kikwete wilayani Muleba.
Wananchi wa Muleba wakimshangilia Rais Jakaya Mrisho Kikwete alipowasili wilayani humo akiwa katika ziara yake ya siku sita Mkoani Kagera.
Rais Kikwete akiongea na viongozi wa wilaya ya Muleba baada ya kupokea taarifa ya maendeleo, akiwa na mawaziri watano anaoongozana nao katika ziara hiyo.
Mbunge wa Muleba akitoa  maoni na kero za jimbo lake.
Waziri wa Uchukuzi Dkt Harrison Mwakyembe akiwahakikishia viongozi wa Muleba juu ya mipango ya serikali kuleta meli za abiria mpya mbili katika ziwa Victoria.
Rais Kikwete akipata maelezo ya mpango kabambe wa maji wilaya ya Muleba.
Rais Kikwete akizindua mradi mkubwa wa maji wilayani Muleba.
Rais Kikwete akikata utepe kuzindua mradi wa maji.
Rais Kikwete akimtwisha ndoo ya maji mmoja wa wananchi wa Muleba baada ya kuzindua mradi mkubwa wa maji kwa wilaya hiyo.
Mwananchi mwingine akitwishwa maji.
Ngoma ya utamaduni ikimlaki Rais Kikwete alipowasili katika mkutano wa hadhara.
Rais Kikwete akisalimia wananchi.
Rais Kikwete akiangalia mazao yatokanayo na uzalishaji mbegu ya kampuni ya Itente ya Muleba.
Rais Kikwete akipozi na wafanyakazi wa kampuni ya uzalishaji mbegu ya Itente.
Rais Kikwete akifurahia ngoma.
Umati wa wananchi Muleba ukimsikiliza Rais Kikwete.
Rais Kikwete akiongea na wananchi wa Muleba.
Rais Kikwete akihutubia wana Muleba.
Sehemu ya umati mkutanoni.
Rais Kikwete akiendelea kungea na wananchi.
Umati  katika mkutano wa hadhara.
Umati katika mkutano wa hadhara.
Rais Kikwete akijiunga na waumini wa Muleba kusali swala ya Magharibi kabla ya kufuturu.
Dua ikisomwa baada ya futari aliyoandaa Rais Kikwete kwa wananchi wa Muleba.
Dua ikiombwa baada ya futari.
Dua.
Wananchi wa Muleba katika futari aliyoandaa Rais Kikwete wilayani Muleba.

0 comments: