Na Makongoro Oging'
KIJANA
mmoja ambaye jina lake halikuweza kupatikana mara moja anayedaiwa ni
mzoefu wa wizi kwa kutumia usafiri wa pikipiki ‘bodaboda’, ameuawa baada
ya kumliza mwanamke aliyetambulika kwa jina la Jusmini.
Tukio hilo lilitokea mwishoni mwa wiki iliyopita maeneo ya Mwenge
jijini Dar, saa tatu usiku ambapo inadaiwa mwanamke huyo alikuwa
akikatiza mitaa hiyo huku akiwa ameweka mkoba wake kwapani.
Ikadaiwa
mwanamke huyo akiwa eneo hilo huku akiamini yuko salama, ilitokea
bodaboda kwa nyuma ikiwa imebeba abiria na ghafla alishangaa
anakwapuliwa mkoba wake.
“Unajua yule mama alikuwa akitembea kwa
kujiamini lakini inavyoonekana wale jamaa ambao ndiyo zao kuwaibia watu
walikuwa wamemlia ‘timing’ tangu aliposhuka kwenye daladala.
“Tuliposikia
makelele ya mwizi, tulimfuata mama huyo na tulipomuuliza akatuambia
ameibiwa mkoba wake huku akituonesha vijana hao ambao muda huo walikuwa
wakikimbia,” kilieleza chanzo hicho kilichoshuhudia tukio zima.
Ikaelezwa kuwa, kufuatia maelezo ya mwanamke huyo, baadhi ya watu
wenye hasira kali wengine wakiwa kwenye pikipiki waliamua kuwakimbiza
wezi hao ambapo mmoja alishuka na kukimbia kivyake huku mwenye bodaboda
akizuiwa kwenye geti kuu ya kutokea magari.
“Alipozuiwa akaona
imeshakua soo, akashuka na kuitelekeza pikipiki yake kisha akataka
kudandia gari nyingine lakini watu wakafanikiwa kumkamata kwenye mataa
ya Mwenge ambapo magari yalisimama, jamaa alishushiwa kichapo hadi
akauawa,” kiliendelea kupasha chanzo hicho.
Baada ya kijana huyo
kuuawa, polisi walifika eneo la tukio na kuuchukua mwili wake. Kamanda
wa Mkoa wa Kipolisi wa Kinondoni, Charles Kenyela (pichani)alipoulizwa
kuhusiana na tukio hilo alisema taarifa za kifo cha kijana huyo
hazijafika mezani kwake lakini akasema anaendelea kufuatilia.
0 comments:
Post a Comment