Tuesday, April 2, 2013

VODACOM FOUNDATION YASAIDIA UJENZI WA KITUO CHA AFYA PEMBA

Mkuu wa Mfuko wa Vodacom wa Kusaidia Jamii - (Vodacom Foundation), Yessaya Mwakifulefule, akikabdhi kwa mmoja wa wazee wa Shehia ya Michenzani Mkoa wa Kusini Pemba mfano wa hundi yenye thamani ya Sh. milioni 30. Fedha hizo zimetolewa kumalizia ujenzi wa jengo la kituo cha afya cha Michenzani ili kurahisisha upatikanaji wa huduma za afya katika eneo hilo. Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Prof. Makame Mbarawa (wa pili kulia) na Meneja Uhusiano wa Nje wa Vodacom Salum Mwalim wakishuhudia.…
Mkuu wa Mfuko wa Vodacom wa Kusaidia Jamii - (Vodacom Foundation), Yessaya Mwakifulefule, akikabdhi kwa mmoja wa wazee wa Shehia ya Michenzani Mkoa wa Kusini Pemba mfano wa hundi yenye thamani ya Sh. milioni 30. Fedha hizo zimetolewa kumalizia ujenzi wa jengo la kituo cha afya cha Michenzani ili kurahisisha upatikanaji wa huduma za afya katika eneo hilo. Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Prof. Makame Mbarawa (wa pili kulia) na Meneja Uhusiano wa Nje wa Vodacom Salum Mwalim wakishuhudia.
Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Prof. Makame Mbarawa akielezea kwa  Mkuu wa Vodacom Foundation, Yessaya Mwakifulefule na Meneja Uhusiano wa Nje wa Kampuni ya Vodacom, Salum Mwalim (mwenye fulana nyekundu) ujenzi wa jengo jipya la kituo cha Afya cha Michenzani Mkoa wa Kusini Pemba muda mfupi kabla ya Vodacom Foundation kukabidhi hundi yenye thamani ya Sh. milioni  30 kumalizia ujenzi wa jengo hilo.
Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Prof. Makame Mbarawa, akiongoza kikundi cha ngoma ya kibati kutoka Chokochoko Mkoa wa Kusini Pemba kucheza ngoma hiyo wakati wa hafla ya kupokea hundi yenye thamani ya Sh. milioni  30 kumalizia ujenzi wa kituo cha Afya cha Michenzani Kisiwani humo zilizotolewa na Mfuko wa Vodacom wa kusaidia Jamii - (Vodacom Foundation). Wa pili kushoto ni Mkuu wa Mfuko huo, Yessaya Mwakifulefule akifurahia burudani hiyo.
---
WAKAZI wa Shehia ya Michenzani, Wilaya ya Mkoani Mkoa wa Kusini Pemba na maneo ya jirani sasa wana kila sababu ya kuwa na uhakika wa huduma za afya kwa ukaribu zaidi kufuatia msaada wa Sh 30 Milioni uliotolewa na kampuni ya Vodacom kupitia mfuko wake wa kusaidia Jamii – Vodacom Foundation kwa ajili ya kuamlizia ujenzi wa jengo jipya la kituo hicho.
Jengo hilo ambalo kwa sasa lipo katika hatua ya linta linajengwa na Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Tenknolojia Profesa Makame Mbarawa akishirikiana na nguvu za wananchi.
Kutolewa kwa fedha hizo ambazo zitanunulia vifaa vya ujenzi vinavyohitajika kwa ajili ya kazi ya kuezeka pamoja na vifaa vingine vya kumalizia ujenzi ni matokeo ya juhudi za makusudi za mfuko huo za kusaidia miradi ya kijamii yenye lengo la kuboresha upatikanaji wa huduma za kijamii kwa wananchi hapa nchini.
Akikabidhi mfano wa hundi kwa wakazi wa Mkanyageni katika hafla iliyoongozwa na Waziri Profesa Mbarawa, Mkuu wa Mfuko huo Yessaya Mwakifulefule amesema Vodacom Foundation imekuwa na dhamira ya dhati ya kusaidia maisha ya watanzania mijini na vijijini ili kuboresha huduma za kijamii ikiwemo elimu, afya na uwezeshaji wanawake  kiuchumi.
“Tunajisikia furaha sana leo kuona Vodacom Foundation ipo hapa Michenzani kuendeleza azma yake ya kuunga mkono juhudi za maendeleo, tutachangia fedha ambazo zitatumika kununulia vifaa vya ujenzi kumalizia ujenzi wa kituo cha afya katika eno hilli.”Alisema Mwakifulefule.
Hata hivyo Mwakifulefule aliwapongeza wakazi wa Shehia ya Michenzani na jimbo zima la Mkanyageni hususan vijana kwa namna wanavyojitolea kushiriki katika miradi ya maendeleo jambo ambalo amesema huenda limechangia kwa kiasi kikubwa kumpa nguvu Waziri Prof;Mbarawa ambae ni mweneyeji  wa eneo hilo kusaidia maendeleo.
“Nimezunguka sehemu mbalimbali hapa nchini hamasa na ari niliyoiona hapa ni ya kipekee jinsi ambavyo wananchi mnavyojitolea katika miradi ya maendeleo hili ni jambo zuri na linawapa moyo wahisani wa maendeleo.”Alisema Mwakifulefuke na kuongeza. “Na sisi katika fedha tutakazozitoa kumalizia ujenzi zinahusisha fedha za kulipia gharama za mafundi na vibarua mbao ni miongoni mwenu. Kwa namna hiyo tunaamini kuwa tutakuwa pia tunaimarisha hali ya uchumi wa vijana wa eneo hili.”
Kwa upande wake Waziri Profesa Mbarawa ameishukuru Vodacom Foundation kwa kukubali kusaidia kumalizia ujenzi wa kituo hicho,
“Nawashukuru Vodacom Foundation kwa kuja hapa na kusaidia maendeleo yetu ila nataka niwaambie wananchi kwamba haya yote hayaji tu hivihivi bali hutafutwa.”   Alisema Profesa Mbarawa
Waziri huyo wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia  aliwashukuru vijana na wakazi wa Mkanyageni kwa jinsi wanavyojitoa na kuwaeleza kuwa hiyo ni silaha muhimu ya maendeleo hivyo waupeke kudanganywa na badala yake waangalie namna gani ya kuleta maendeleo na kiwanga mkono wale wanaowaletea maendeleo badala ya kukubalia hila za kuwabeza.
Vodacom Foundation imekuwa ikichangia miradi mbalimbali ya maendeleo Zanzibar ambapo pia hivi karibuni imeahidi kutoa boti mbili za uvuvi kwa vikundi vya vijana Pemba na Unguja kusaidia juhudi za serikali ya Zanzibar za kutengeza ajira kwa vijana.
Mbali na mchango huo, Mwishoni mwa mwaka jana, Vodacom Foundation ilisaidia wanawake wajasiriamali zaidi ya 300 kwa kuwaptia mikopo nafuu isiyo na riba wala dhamana yenye thamani ya zaidi ya Sh. 27 Milioni katika kisiwa cha Unguja pamoja na kuahidi kuchangia Sh 15 Milioni kwenye mfuko wa maendeleo ya watu wenye ulemavu Zanzibar.

0 comments: