Saturday, March 23, 2013

Zitto Kabwe: TaifaStars ninyi ndio tumaini letu kubwa

 Zitto-Kabwe-akikokota-mpira1 23190
TaifaStars ninyi ndio tumaini letu kubwa wakati huu nchi yetu imejaa changamoto nyingi na kukata tamaa. Wakati Umoja wa Taifa upo mashakani, ninyi mnatufanya tuvae na kupeperusha Bendera yetu nzuri ya Taifa. Dakika tisini uwanjani Tanzania inakuwa moja, ushindi hutupa fahari kubwa na kusahau vyama vyetu, Dini zetu, madaraja ya Maisha nk. Ingieni uwanjani Kwa ufahari mkubwa. Tupeni raha #TaifaStars #TZBrazil2014
Nimezungumza kwa simu na nahodha wa Timu ya Taifa, #TaifaStars Tanzania one @JumaKaseja . Morale ya Vijana wetu ipo juu sana. Wanaomba mjae uwanjani na kuwashangilia Kwa Nguvu. Kila Mtu ashike Bendera ya Taifa au Rangi za Bendera ya Taifa. Mliopo Dar msituangushe, uwanja wa Taifa ujae pomoni. #Nyumbani tushinde. Ushindi Ni lazima. Go stars Go

0 comments: