Saturday, March 23, 2013

Waziri Sitta awaanika wabunge wa Afrika Mashariki kuhusu posho


Na: Gustav Chahe, Iringa
MTU mmoja amenusurika katika ajali baada ya gari alilokuwa akisafiria kuacha njia na kutumbukia kwenye mtaro wa maji. Ajali hiyo imetokea majira ya saa 11 alfajiri katika barabara ya Iringa – Dodoma maeneo ya Sabasaba katika Manispaa ya Iringa ambapo gari lenye namba za usajili T 287 AAG Prado limetumbukia kwenye mtaro kwa kile kilichoelezwa kuwa chanzo cha ajali hiyo ni
hitilafu katika maungio ya tairi (boll joint).
Kwa mujibu wa maelezo yaliyotolewa na kikosi cha uokoaji (K.B. WORKSHOP) zinasema kuwa baada ya kupata hitilafu katika tairi moja, gari lilipoteza mwelekeo na kuhama njia kasha kutumbukia kwenye mtaro.
Imeelezwa kuwa katika gari hilo alikuwemo dereva pekee ambapo hata hivyo hakupata majeraha makubwa.
Gari hilo lilikuwa likitokea mjini Iringa kuelekea Kihesa ambapo mara baada ya ajali hiyo imeelezwa kuwa dereva alikwenda kupumzika kutokana na maumivu ya majeraha aliyopata japo kuwa jina lake halikutajwa.
Mtandao huu umeshuhudia gari lenye namba za usajili T 332 AKP mali ya K.B.WORKSHOP wakiokoa gari hilo lililokuwa kwenye mtaro.

0 comments: