Thursday, March 7, 2013

WANAWAKE WASHEREKE SIKU YAO KWA KUPEWA KIPAO MBELE

1 93513
Ofisa Mawasiliano Mwandamizi, Mradi wa CHAMPION, Muganyizi Mutta akitoa mafunzo kwa waandishi wa habari wa mkoa wa Iringa katika ukumbi wa royal hotel mafinga wiki hii.
Na Denis Mlowe, Iringa
WANAHABARI nchini wametakiwa kuandika habari zinazolenga kukuza usawa wa jinsia katika vyombo vyao vya kazi.
Ofisa Mawasiliano Mwandamizi, Mradi wa CHAMPION, Muganyizi Mutta alisema hayo wiki hii wakati wa mafunzo ya wanahabari mkoani Iringa yaliyofanyika kwenye ukumbi wa Hoteli ya Royal Park mjini Mafinga.Mutta alisema, uwiano wa habari zinazoripotiwa na vyombo vya habari nchini kuhusiana hauko sawa hivyo kushindwa kufikia malengo ya uwiano wa nusu-kwa-nusu ambao unahimizwa kwa sasa kote ulimwenguni.Alisema, vyombo vingi vya habari kuanzia magazeti, televisheni na radio kwa asilimia kubwa vimebeba habari za wanaume kuliko wanawake, jambo ambalo linapaswa kubadilika.


“Vyombo vingi vya habari vimeegemea katika habari ambazo hazina usawa kwa upande wa wanawake kuanzia kwenye habari zenyewe, picha zanazochapishwa na matangazo ambayo yameegemea upande wa jinsia ya kiume,” alisema.

Mutta alisema, tofauti ya uwiano huo inaanzia ngazi za chini katika jamii hadi kwenye sekta nyingine, hivyo kuwataka wanahabari kuondokana na mtazamo huo hasi ambao haulengi kuleta usawa na zaidi humbagua mwanamke.

Aidha, alitoa mfano wa vichwa vya habari vinavyotumika katika vyombo vingi vya habari, hususan magazeti, ambavyo vinamuonyesha mwanamke kama ndiye mwathirika mkubwa katika masuala yote ya ujinsia.

“Kati ya vitu vinavyokuwa na tofauti ni katika kuchagua vichwa vya habari, picha zinazochapishwa katika vyombo vya habari, sentensi zinazotumika na maneno vinaonyesha ni kiasi gani mwanamke anabaguliwa katika vyombo vya habari” alisema Mutta

Naye Paulina Kuye mwandishi wa habari wa radios Nuru Fm alisema kwamba wanawake wengi wanakosa kujiamini katika kufanya kazi za uandishi wa habari na kukata tamaa kutokana na kutokukubali kukosolewa.

“Sisi wanawake pia tunachangia sana kuwa wachache katika tasnia ya habari na kutojiamini kwetu nacho ni chanzo kikubwa sana kufanya fani hii kutawaliwa na wanaume” alisema Kuye.

0 comments: