Saturday, September 14, 2013

Rais Dk. Shein amtembelea Padri aliyemwagiwa Tindikali Mjini Unguja


IMG_4338
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein akisalimiana na Padri Joseph Monesmo Magamba wa Kanisa la Romani Katoliki Parokia ya Machui, alipofika katika Hospitali ya Mnazi Mmoja kumpa pole Mjini Unguja,baada ya kumwagiwa tindikali na watu wasiojulikana katika Mtaa wa Mlandege Mkoa wa Mjini Magharibi jana jioni, Padri alimwagiwa Tindikali alipokuwa akitoka kupata huduma ya Mtandao.
IMG_4342
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akimsikiliza Padri Joseph Monesmo Magamba,wa Kanisa la Romani Katoliki Parokia ya Machui,akitoa maelezo jinsi alivyopata mkasa wa kutiwa  Tindikali jana na watu wasiojulikanwa,katika mtaa wa Mlandege Mjini Unguja, alipofika katika Hospitali ya Mnazi Mmoja kumpa pole,ambapo amelazwa na kuapatiwa matibabu.
IMG_4349 (1)
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akiwafariji jamaa  na ndugu wa Padri Joseph Monesmo Magamba,wa Kanisa la Romani Katoliki Parokia ya Machui,waliofika katika Hospitali ya Mnazi Mmoja kumpa pole Padri huyo baada ya kumwagiwa Tindikali na Watu wasiojulikanwa jana jioni Mtaa wa Mlandege Mjni.
IMG_4360
Mmoja wa Ngugu wa Padri Joseph Monesmo Magamba wa Kanisa la Romani Katoliki Parokia ya Machui akimueleza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,hisia zake kwa Uchungu kutokana na kitendo hicho cha kumwagiwa Tindikali na watu wasiojulikanwa  kwamba zilichukuliwe hatua za kisheria na kukomeshwa Vitendo kama hivyo.
IMG_4370
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akifafanua jambo wakati akiwafariji jamaa na ndugu wa Padri Joseph Monesmo Magamba wa Kanisa la Romani Katoliki Parokia ya Machui,waliofika kumuangalia Padri huyo aliyelazwa katika Hospitali ya Mnazi Mmoja baada ya kumwagiwa Tindikali na Watu wasijulikanwa jana jioni katika Mtaa wa Mlandege Mjini Unguja.(Picha na Ramadhan Othman wa Ikulu, Zanzibar).

0 comments: