Monday, April 22, 2013

Taswira:Waziri Mkuu Mstaafu Edward Lowassa Akabidhiwa Tuzo Ya Heshima Mkoani iringa

 Askofu  wa  kituo  cha maombezi  na uponaji cha  Overcomers Power Center (OPC) Dkt  Boaz Sollo (kushoto) akimakabidhi tuzo ya  heshima mfano  wa ramani ya  Tanzania  waziri mkuu  wa zamani Edward  Lowassa  jana katika hafla ya  kuchangia ujenzi  wa kanisa na kuendeleza kituo cha radio Overcomers Fm ,katika harambee  hiyo Lowassa aliahidi kuachangia milioni 15  na kufanikisha kupata  Tsh zaidi ya milioni 75 zikiwemo  fedha taslimu na ahadi .
  waziri mkuu  wa zamani Edward  Lowassa akionyesha tuzo ya  heshima mfano  wa ramani ya  Tanzania aliyotunukiwa, kushoto kwake ni Askofu  wa  kituo  cha maombezi  na uponaji cha  Overcomers Power Center (OPC) Dkt  Boaz Sollo Mheshimiwa Lowassa Alikabidhiwa Tuzo Hiyo katika hafla ya  kuchangia ujenzi  wa kanisa na kuendeleza kituo cha radio…
 Askofu  wa  kituo  cha maombezi  na uponaji cha  Overcomers Power Center (OPC) Dkt  Boaz Sollo (kushoto) akimakabidhi tuzo ya  heshima mfano  wa ramani ya  Tanzania  waziri mkuu  wa zamani Edward  Lowassa  jana katika hafla ya  kuchangia ujenzi  wa kanisa na kuendeleza kituo cha radio Overcomers Fm ,katika harambee  hiyo Lowassa aliahidi kuachangia milioni 15  na kufanikisha kupata  Tsh zaidi ya milioni 75 zikiwemo  fedha taslimu na ahadi .
  waziri mkuu  wa zamani Edward  Lowassa akionyesha tuzo ya  heshima mfano  wa ramani ya  Tanzania aliyotunukiwa, kushoto kwake ni Askofu  wa  kituo  cha maombezi  na uponaji cha  Overcomers Power Center (OPC) Dkt  Boaz Sollo Mheshimiwa Lowassa Alikabidhiwa Tuzo Hiyo katika hafla ya  kuchangia ujenzi  wa kanisa na kuendeleza kituo cha radio Overcomers Fm ,katika harambee  hiyo Lowassa aliahidi kuachangia milioni 15  nakufanikisha kupata  Tsh zaidi ya milioni 75 zikiwemo  fedha taslimu na ahadi .Picha na Habari na Mdau Francis Godwin
--
WAZIRI  mkuu  mstaafu  Edward  Lowassa amesema kuwa mbali ya  kuwa  yeye  si tajiri ila bado ataendelea  kufanya kazi  yake kwa  ukaribu  zaidi na jamii  ikiwa ni pamoja na kushirikiana na  marafiki  zake  kusaidia na kuwataka  wale  wote  wenye kusema dhidi yake  kuendelea  kusema ila hatarudi  nyuma katika kutoa misaada kama njia ya  kutafuta baraka za Mungu.
Lowassa ambae  pia alikabidhiwa   tuzo ya  heshima kwa ajili ya  kuendeleza  kulipigania  Taifa  la Tanzania ,huku  mwenyewe akichangia kiasi cha Tsh milioni 15  na mbunge  wa jimbo la Ludewa  Deo Filikunjombe akichangia  milioni 9  kati  ya  fedha  zote  zaidi ya Tsh milioni 75 zilizochangwa kwa ajili ya   kuendeleza ujenzi  wa kanisa la OPC mkoani Iringa kama njia ya  kuhamasisha amani katika Taifa ametaka  watanzania  kuwapuuza  wale  wote wanaoeneza siasa  za uchochezi .
“Nataka  kuwaomba  leo wachukieni  wachochezi na pia niwaelezeni  kuwa mimi  si tajiri ila nina utajiri  wa  watu na ushawishi na ninafanya  mambo haya ili kumbukumbu yangu  iweze  kuandikwa  Mbinguni  na nimekuwa  nikialika watu  wengi  na nimekuwa nikifika   wacha  wenye  kusema waseme  watasema ila usiku  watalala wenyewe ….sitaacha  kusaidia kwa kuogopa kusemwa”
Akizungumza katika hafla  hiyo  iliyoandaliwa na kituo  cha maombezi na uponyaji mkoani Iringa Overcomers Power  Center (OPC) na kufanyika katika  ukumbi  wa St Dominic mjini Iringa leo  Lowassa  alisema kuwa yeye  si tajiri kama ambavyo  watu  wanavyofikiri ila amekuwa akipewa  nguvu na rafiki  zake ambao  wamekuwa  wakimuunga mkono pindi anapoalikwa katika hafla  mbali mbali.
“Nataka  kwanza  kuwashukuru  ndugu zangu  wa mkoa  wa Iringa na napenda  kumshukuru  zaidi Askofu Dkt  Boaz Sollo kwa kunialika  mkoani Iringa …..ila napenda  kuwaeleza  kuwa  si kwamba nachangia michango mbali mbali katika jamii kama mimi ni tajiri  ila mimi ni mtumishi nisiye na faida na nayaweza yote  katika  yeye anitiaye nguvu Pia  nawashukuru  sana  wabunge  wenzangu ambao  wamepata  kushiriki name  leo katika  ziara  hiyo  akiwemo  mbunge machachari  bungeni Deo  Filikunjombe , Kagi Lugola  na dada yangu  Ritta Kabati  bila kumsahau mbunge Mendradi Kigola kwa kuungana nami leo naamini nao  wamepanda  mbegu  bora”.
Lowassa  alisema kuwa anatambua  bado ana mialiko migi  sana na lazima anaifanyia kazi mialiko yote kama ambavyo jamii imepata  kumwalika na kuwa hata  hatua ya  mkoa  wa Iringa kumpa  tuzo hainamanishi  kuwa ni mwisho wa  yeye  kualikwa.
Hata  hivyo  Lowassa  alisema  kuwa  kwa upande  wake anapongeza  jitihada za askofu Dkt  Sollo kwa  kuwa na mipango na mitazamo ya  kulisaidia  Taifa  kwa kuanzisha  ujenzi  wa kanisa kwa ajili ya  kudumisha amani na  kwenda mbali  zaidi kwa  kuanzisha  kituo cha  radio  Overcomers  Fm   chambo ambacho  kitatumika  kudumisha amani ya mkoa wa Iringa na Taifa  pia
Kuhusu amani ya Taifa  la Tanzania  LOwassa alisema  kuwa alikuwa ni miongoni mwa watu  walioalikwa Kenya  katika sherehe ya  kuapishwa Rais mpya wa Kenya  Uhuru Kenyatta ila  sehemu kubwa ya  wote  waliotoa  salam zao  walitumia muda mwingi kupongeza  vyombo vya habari kwa kulinda amani na hivyo  kuvitaka  vyombo  vya habari za Tanzania na wanahabari  kuendelea  kuandika habari bila kuhatarisha amani ya Taifa
“Tusiruhusi amani ya nchi  yetu  iyumbishwe na mtu  awaye  yeyote  na kila mtanzania anapaswa  kulinda amani  hii  kwa nguvu  zote ….Nawaombeni  wanahabari  tunzeni amani  yetu…wapuuzeni  wale  wote  wanaoch0chea machafuko katika Taifa  hili ….tuachane na  udini  wala ukabila katika  taifa  letu  ila  “
Katika  hatua  nyingine  Lowassa  aliwapongeza  wabunge wa CCM ambao  wameendelea  kupigania wanyonge  bungeni akiwemo  Deo Filikunjombe mbunge wa Ludewa na mbunge wa jimbo la Mwibara Kagi Lugola  kuwa ni miongoni mwa wabunge ambao  amekuwa akiwapenda kutokana na kusema kweli  bungeni.
Kwa upande  wake mbunge  Filikunjombe alisema kuwa mbali ya kutoa ahadi ya  kuchangia  kiasi cha Tsh milioni 9 ila bado atamwalika  Lowassa  jimboni kwake  Ludewa na kuwa kanisa  hilo la OPC halijakosea  kumpa tuzo ambayo ni ramani  ya  Tanzania kutokana na Lowassa kuwa ni mtu  wa  watu mpendwa na  watu na kuwa tuzo  hiyo  ina maana kubwa na hawajakupa ramani ya jimboni kwako Monduli  
Filikunjombe  alimtaka  Lowassa  kuendelea  kuchapa kazi na  kuwa hajakosea  kuwaalika  wao kwani bungeni  kuna  wabunge  zaidi ya  300 ina amewachagua wao  pekee ni jambo la kumshukuru  na  kumfananisha L0wassa  na mti  unaopigwa mawe  kuwa ni mti wenye matunda
“Nakuomba  Lowassa simama Imara  sisi  wana Iringa  tupo nyuma yako na niseme  tuna kazi kubwa ya kuifanya katika Taifa  hili kubwa ni  kumwomba Mungu na makanisa na dini  zote  kuungana katika maombi  zaidi kwani  vita  ni kubwa mbele “
Kwa  upande  askofu  Dkt  Sollo  mbali ya  kumpongeza Lowassa bado  alisema kuwa  wao kama kanisa wataendelea  kumwombea  afya njema na kuona kuwa mambo yake yanafanikiwa na ndio maana ya kumpa  tuzo  hiyo  ya heshima.
Sollo alisema kuwa mchango  wa TSh milioni 15  ulioahidiwa na Lowassa na ule  wa milioni 9  ulioahidiwa na mbunge wa jimbo la Ludewa Deo  Filikunjombe ni mchango ambao  wao wanaupongeza na kuwapongeza  wabunge  wengine akiwemo Ritta Kabati aliyeahidi Tsh milioni 2 ,Benki ya  wananchi Mufindi milioni 2 , mwenyekiti  wa CCM mkoa  wa Iringa Jesca Msambatavangu milioni 2  mfanyabiashara Salim Abri milioni  1 na wengine  wengi ambao  wamepelekea  kupata  zaidi ya Tsh milioni zaidi ya 75  pesa taslim na ahadi .

0 comments: