Tuesday, March 5, 2013

NDOTO ZA MACHESTER UTD KUTWAA TAJI LA ULAYA ZAISHIA KATIKA MJADARA MKUBWA ULAYA


FERGUSON ASUSIA WANAHABARI KISA KADI NYEKUNDU


Manchester United's Nani

Kocha wa Manchester United  Sir Alex Ferguson hakuwa tayari kuzungumza na vyomb vya habari ,baada ya timu kusukmwa nje ya ligi ya mabingwa barani ulaya Dhidi ya   Real Madrid katika uwanja wa   Old Trafford.
Ferguson alishindwa kumvumilia  mwamuzi kutoka uturuki Cuneyt Cakir baada ya kumpa kadi nyekund Nani baada ya kumfanyia rafu mbaya  Alvaro Arbeloa katika dakika ya  56 wakati United ilikuwa ikongoza kwa goli la kujifunga la  Sergio Ramos's. 
Sir Alex Ferguson
Kocha msaisizi wa United  Mike Phelan alimwakilisha Feg  katika mahojiano baada ya mechi kumalizka  : "Chumba cha kubadilishia sio salama kwetu Kocha mkuu amekasirsihwa na maamuzi ya mwamuzi wa leo ndio maana hayuko hapa .
na mimi ndiye nitakaye zungumza 
 
"Sidhani kama mkufunzi mkuu atakuwa sawa kuzungumza .
Naongea haya ili muone ni kwa jinsi gani tumesikitishwa hii ni klabu kubwa duniani  ."
Phelan : "Tumesikitishwa na kuumia sana tuna mashaka kwanini limetokea na kwa sababu gani limetokea .
 sio rahisi mkiwa kumi kiwanjani mkacheza na real Madrid .
" Waamuzi wapo kiwanjani ili kufanya Maamuzi lakini unatakiwa kufanya maamuzi ya maana . 
Najua vyombo vya habari na watazamanji duniani  kote wametazama hili na watakuwa na maoni tofauti lakini tumesikitishwa sana."

NDOTO ZA MACHESTER UTD KUTWAA TAJI LA ULAYA ZAISHIA KATIKA MJADARA MKUBWA ULAYA

Cristiano Ronaldo of Real Madrid reacts after scoring his team's second goal during the UEFA Champions League Round of 16 Second leg match between Manchester United and Real Madrid 
Ndoto za Manchester United's kutwaa ubingwa wa ulaya zimemalizka kwa mjadara mkubwa huku kocha Man u    Sir Alex Ferguson na wachezaji wakikiona kiwanja cha OT ni Kikubwa kuliko wakati mwingine.
United walionekana tayari wameanza kuingia hatua ya Robo fainali mara baada ya kipindi cha pili Kuanza huku  Real Madrid's ikijitia matatani mara baada ya Sergio Ramos's kujifunga mwenyewe na kuipa goli United  ambalo ilikuwa likichagizwa na sare ya goli moja kwa moja  katika mchezo wa kwanza uliofanyika  Bernabeu. 
Man Utd v Real Madrid
Lakini mchezo ulibadilika baada ya Mwamuzi kutoka Uturuki  Cuneyt Cakir's Kumlima kadi nyekundu Luis  Nani baada ya kumchezea vibaya Mchezaji  Real Madrid Alvaro Arbeloa katika dakika ya  56  - kadi ambayo iliwanyong'onyesha wachezaji wa United .
Vijana wa Jose Mourinho's , waliongeza bidii , na kutumia pengo la hilo ambapo mchezaji wa zamani na kiungo wa Tottenham  Luka Modric na kijana wa zamani wa Timu hiyo   Cristiano Ronaldo walitumia dakika sita kusawazisha na kufunga goli la ushindi na kusonga mbele katika hatua Robo fainali .
Man Utd v Real Madrid
Baada ya luis Nani Kupewa kadi nyekundu Ferguson's alinoneka kuto kuamini kinachotokea na kumshutumu  mwamuzi kuwa hakutenda haki  baada kutolewa mchezaji wake  .
Mourinho sasa atakuwa analisaka taji la tatu la ligi ya mabingwa barani ulaya akiwa na klabu tatu tofauti  wakati Manchester utd wanatakiwa kujikita katika makombe ya nyumbani ambapo jumapili watakuwa wakipambana na chelsea katika kombe Fa huku wakiwa wanaongoza alama 12 dhidi ya bingwa mtetezi Manchester city .
 
Huenda mwaka huu ukawa kama 1996, ambapo England haikuwa na timu yoyote kwenye hatua ya robo fainali, kwani Chelsea na Manchester City walishatolewa na Arsenal wapo ukingoni wanapoelekea Ujerumani wiki ijayo.

Baada ya mechi Rio Ferdinand alimwendea mwamuzi na kujidai kumpigia makofi kana kwamba anampongeza, bila shaka kuonesha kuudhiwa na uamuzi wake wa kumpa kadi nyekundu Nani, na pengine kuwanyima penati kadhaa walizodhani walistahili.




0 comments: