Tuesday, March 12, 2013

Manyara Yashinda Tuzo ya Vipaji Miss Utalii 2013

 
Mshindi wa Miss Utalii Vipaji kutoka Mkoa wa Manyara wa kati kati akiwa na washindi wenzake wawili waliofika mpaka Tatu bora
HATIMAYE Mshiriki wa Miss Utalii Tanzania 2012/13 kupitia Mkoa wa Manyara ameshinda tuzo ya vipaji 2012/13 na kuibwaga mikoa mingine 29 ya Tanzania Bara na Zanzibar. Mrembo Miss Mary (19) alionesha kipaji cha hali ya juu katika ushindani ambao ulikuwa mkubwa hasa kutoka kwa warembo wa mikoa ya Lindi, Kagera, Dodoma, Zanzibar na Katavi.
Hata hivyo, mchuano ulikuwa mkali zaidi kati ya Miss Utalii, Lindi Manyara na Kagera ambao walionesha Umahili mkubwa wa kucheza ngoma za asili na kupelekea kuingia katika hatua ya Tatu Bora. Katika Hatua hiyo ya Tatu Bora washiriki hao walicheza wimbo mmoja ujulikanao kwa jina la katope kutoka kundi la ngoma za asili la kibiriti ambao ni mchanganyiko wa ngoma mbalimbali wa makabila ya ngoma za kusini.

Mshindi wa Tuzo la Vipaji akiwa anafuraha Muda Mchache baada ya kutangazwa kuwa yeye ndiye mshindi.

Hali hiyo iliwafanya wapenzi wa fani ya urembo waliofurika katika ukumbi wa Dar Live Mbagala kuto kuamini kwamba wanao cheza jukwaani ni Mabinti wa Kizazi kipya ambao kwa Hali ya kawaida ya sasa ni nadra sana kumuona sister Duu tena Mrembo kucheza ngoma za asili kwa ufasaha na umahili mkubwa. Wapenzi hao walijikuta wakiacha viti vyao na kuanza kushangilia kwa nguvu mwanzo hadi mwisho huku wakiwapongeza waandaaji wa shindano la Miss Utalii Tanzania kuwa ni Hazina kubwa ya utamaduni wa Mtanzania na Wengine wakithubutu kusema Miss Utalii ni mtambo wa kurekebisha tabia kwa kuweza kuwabadirisha fikra za mabinti hao wa kizazi kupya mashindano hayo kwa ya kuwa kucheza ngoma za asili ni ushamba hadi kuwafanya kuwa wacheza ngoma mahili tena hadhalani bila ya Aibu na kwa kujivunia utamaduni na Ngoma za Asili Tanzania.
Wapenzi hao waliohudhuria katika shindano hilo wakisika kwa nyakati tofauti kuitaka na kuishauli Serikali na mamlaka za utalii kudhamini shindano la Miss Utalii Tanzania kwa Faida ya Jamii na Taifa kwani shindano hili limedhihilisha uwezo mkubwa wa sio tuuu kuhifadhi utamaduni wa mtanzania bali pia kuhamasisha na kutangaza utalii wa tanzania kitaifa na kimataifa.
“Shindano hili ni zuri na ni lakipekee lakini tatizo inaonekana waandaaji hawajapata wadhamini wa uhakika, kwanini Serikali isiwasaidie hawa,” alisema Jafary Shaibu mpenzi ma mashindano ya urembo.
Akizungumza katika Shindano hilo ambalo Mwanamuziki wa Kimataifa Che Mundugwao alikonga nyoyo za watu kwa Muziki wake wenye asili ya kitanzania, Mgeni Rasmi, Maabad Suleiman Hoja Mustahiki Meya wa Manispaa ya Temeke aliwapongeza sana washiriki na washindi lakini alitoa shukurani za pekee kwa waandaaji wa mashindano haya kwa kuipa manispaa na wilaya ya Temeke Heshima kubwa ya kuwa wenyeji wa Tukio hili la kitaifa lenye hadhi ya kimataifa.
Kiongozi huyo alisema Manispaa ya Temeke na Wilaya inayouwezo wa kuwa wenyeji wa matukio makubwa ya kimataifa na kitaifa kama la Miss Utalii Tanzania 2012/13, hivyo kutoa fursa ya pekee kwa Temeke kujitangaza kiutalii, kitamaduni na kiuwekezaji ndani na nje ya Nchi. Pia aliahidi kuwa Manispaa ya Temeke kuendelea kuunga mkono kwa hali na mali ili kufanikisha fainali hizo ambazo zitafikia kilele katika ukumbi wa Dar Live Mbagala Dar es Salaam.
Mshindi wa Tuzo hiyo ya Vipaji ambaye alishangiliwa na washiriki wote baada ya kutangazwa kama mshindi, alizawadiwa udhamini wa kusoma kozi ya Kiwango cha Diploma katika chuo chochote nchini.
Fainali za Taifa za Miss Utalii Tanzania mwaka huu Zimedhamiwa na: Mtwana Catering Services, Ikondolelo Lodge, Zizou Fashion, Coca Cola Kwanza, VAM General Suppries Limited,Global Publishers, TANAPA, Ngorongoro Crater, Lakeland Africa, Clouds Media Group, Star Tv, Vailey Spring,Dotinata Decoration,Tone Multimedia Group, Baraza la sanaa la Taifa (BASATA )

0 comments: