Thursday, April 25, 2013

LOWASSA CHUPUCHUPU…

Stori: FRANCIS GODWIN, IRINGA

KIJANA ambaye amekuwa ‘akiwaliza’  watu wakiwemo viongozi serikalini kwa kutumia jina la Waziri William Lukuvi aliyejulikana kwa jina moja la Jonathan amenaswa na polisi.
 Mtuhumiwa akiwa chini ya ulinzi baada ya kutiwa mbaro na polisi
Ishu hiyo ilitokea Jumapili iliyopita katika hafla ya Kanisa la Overcomers FM la Askofu Dk. Boaz Sollo kwenye Ukumbi wa St. Dominic…
Stori: FRANCIS GODWIN, IRINGA
KIJANA ambaye amekuwa ‘akiwaliza’  watu wakiwemo viongozi serikalini kwa kutumia jina la Waziri William Lukuvi aliyejulikana kwa jina moja la Jonathan amenaswa na polisi.
Mtuhumiwa akiwa chini ya ulinzi baada ya kutiwa mbaro na polisi
Ishu hiyo ilitokea Jumapili iliyopita katika hafla ya Kanisa la Overcomers FM la Askofu Dk. Boaz Sollo kwenye Ukumbi wa St. Dominic mjini Iringa ambapo kijanna huyo alitaka kumtapeli Waziri Mkuu Mstaafu, Edward Lowassa (pichani) kupitia harambee iliyokuwa ikifanyika kanisani hapo.
Kijana akiwa katika ulinzi mkali wa Askali kanzu wakiwa wana mpeleka kituoni kwa maojiano zaidi

Kijana huyo alipita mbele na MC wa shughuli hiyo alimpa kipaza sauti ambapo alianza kwa kujitambulisha jina na kuongeza yeye ni mtoto wa Lukuvi.
Alisema mara kwa mara amekuwa akimpigia simu Lowassa ili azungumze naye akitaka msaada ambao hakuutaja ukumbini hapo.
Huku Mheshimiwa Lowassa akiwa amesimama wima na kumsikiliza kwa umakini, Jonathan alimwambia siku za nyuma katika mkutano  wa mheshimiwa huyo uliofanyika Viwanja vya Jangwani,  jijini Dar es Salaam alizungumza naye kuhusu shida yake kwa hiyo siku hiyo alitaka atekelezewe.
Kufuatia utambulisho huo, baadhi ya watu waliowahi  kutapeliwa na kijana huyo, akiwemo Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa, Teresia Mahongo waliguna, hali iliyosababisha polisi  kujitokeza na kumtia mbaroni kijana huyo ambaye ilionekana alikuwa akiweka mtego wa kumtapeli Lowassa na  viongozi wengine katika hafla hiyo.
Kada wa CCM mkoani Iringa, Godfrey Malenga  Lukuvi alisema kijana  huyo amekuwa akitumia  jina la waziri kuliza  watu. Alisema wengi  wameshalalamika kuhusu  utapeli unaofanywa na Jonathan na kuna wakati alikamatwa na polisi lakini akaachiwa.
Kwa upande wake, Katibu wa Mbunge  Jimbo la Isimani ambaye pia ni familia ya mheshimiwa Lukuvi,  Thom Malenga Lukuvi alisema amekuwa akipokea malalamiko kutoka kwa watu mbalimbali ambao  wamelizwa na Jonathan na ameshaweka mitego ya kumnasa lakini hakuwahi kufanikiwa.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa, Mahongo alimweleza mwandishi wa habari hizi kuwa Jonathan aliwahi kufika ofisini kwake kwa lengo la kumtapeli lakini alimshtukia na kumpigia simu Waziri Lukuvi ambapo alisema kijana huyo ni tapeli.
Mwandishi wetu alimtafuta Lukuvi kwa simu na alipopatikana alimkana kijana huyo kwamba hamtambui wala hana undugu na ukoo wake.
“Huyu kijana simtambui na wala si ndugu yangu, ila amekuwa akitumia jina langu kutapeli watu na tayari amekamatwa na polisi kwa utapeli huo,” alisema Lukuvi.


0 comments: