Monday, April 8, 2013

ASANTE FAMILIA YA MAREHEMU KANUMBA KWA HII TUZO.

.
Jana April 7 2013 bila kufahamu kitakachotokea nilikwenda viwanja vya Leaders kwa ajili ya kupiga picha na kuchukua habari kwa ajili ya AMPLIFAYA ya Clouds FM na millardayo.com ambapo nilipokua kwenye stage na Camera yangu nikichukua matukio wakati familia ya Marehemu Kanumba ikitoa tuzo mbalimbali kwenye kumbukumbu ya mwaka mmoja ya kifo cha Kanumba, ghafla nikiwa sijategemea… nikawa mtangazaji pekee na mwandishi wa website nilieitwa na kupewa hii tuzo ya familia hiyo kutambua mchango wangu, asante sana kwa familia hii, asante kwa watu wangu wote wa nguvu wanaonisupport.
.
Meya wa Kinondoni, mimi na Mama Kanumba ambapo hii inakua tuzo ya pili millardayo.com kupata lakini ni tuzo ya tatu mimi kama Millard kuipata.
.
.
.
Asanteni kwa love watu wangu wa nguvu, asanteni sana.

0 comments: