STAA
wa muziki wa taarab na mkurugenzi wa Mashauzi Classic, Aisha Ramadhan
‘Isha Mashauzi’ ameibua gumzo na kushangaza mashabiki baada ya kukiri
kuwa yeye ni mtumiaji wa pombe kali na madawa ya kulevya aina ya
mirungi
Ishu hiyo ilijiri Alhamisi ya wiki iliyopita wakati akihojiwa na
mtangazaji wa Redio Times FM, Hadija Shaibu ‘Dida’ kupitia kipindi chake
cha Mitikisiko ya Pwani ambapo alisema mirungi na pombe kali ndiyo
starehe yake kwani inampa stimu kabla hajapanda jukwaani na katika
maisha yake ya kawaida nje ya usanii.
Mashauzi alifunguka hayo baada ya Dida kumtaka atoe ufafanuzi juu ya skendo ya kuvuta bangi inayomkabili ambapo alisema siyo kweli kwamba anavuta bangi ila akakiri kuwa anakula sana mirungi na kugida ulabu. Aliongeza kwamba kwa kuwa hana mume, mtoto wala hataki kuwa na familia, mirungi na pombe ndiyo vitu vinavyompa furaha maishani mwake.

0 comments:
Post a Comment